KIKAO KAZI CHA 4 CHA SERIKALI MTANDAO KUFANYIKA FEBRUARI JIJINI ARUSHA

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), inatarajia kufanya kikao kazi cha nne (4) cha Serikali Mtandao Februari 6 hadi 8, mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.Akizungumza ofisini kwake jijini Dodoma, Meneja Mawasiliano wa e-GA Bi. Subira Kaswaga amesema, lengo la kikao kazi hicho ni kuwakutanisha wadau wa Serikali Mtandao kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ya umma, ili kujadili jitihada mbalimbali...