BARAZA LA MAWAZIRI SASA KIDIJITALI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), amesema kuwa matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Baraza la Mawaziri (e-Cabinet), unalenga kurahisisha utendaji kazi wa baraza hilo sambamba na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.Mhe. Majaliwa amesema hayo Novemba 11 mwaka huu, wakati akifunga Mkutano wa Kazi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri, kuhusu matumizi ya mfumo wa e-CABINET, uliofanyika katika ukumbi wa...