SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO (e-GA)

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuuona Mwaka Mpya wa 2025, kwa niaba ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), napenda kuwatakia nyote Heri ya Mwaka Mpya 2025.Mamlaka ya Serikali Mtandao, inapenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiwezesha e-GA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.Katika mwaka uliopita (2024), e-GA imeweza kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuratibu, kusimami...