e-Mrejesho V2 Kinara wa Tuzo ya WSIS 2025

Tanzania kupitia Mfumo wa e-Mrejesho toleo la pili (e-MrejeshoV2) imeibuka mshindi katika kipengele cha Serikali Mtandao, kwenyeTuzo za Mkutano wa Dunia wa Jumuiya ya TEHAMA mwaka 2025 (World Summit on the Information Society -WSIS 2025). Utoaji wa tuzo za WSIS umefanyika Julai 7 katika mkutano wa Tukio la Ngazi ya Juu la Jukwaa la WSIS+20 (WSIS+20 Forum High-Level Event), unaofanyika mjini Geneva USWIS kuanzia tarehe 7 hadi 11 Julai mwaka huu...