Mfumo wa Ofisi Mtandao (GeOS)

Mfumo wa Ofisi Mtandao (GeOS)

Mfumo wa Ofisi Mtandao umetengenezwa ili kuwezesha na kurahisisha shughuli za utawala za kila siku ndani ya Serikali. Shughuli hizo zinahusu mzunguko wa mafaili na nyaraka ndani na miongoni mwa taasisi za umma.Mfumo huu unapatikana kupitia https://eoffice.gov.go.tz kwa taasisi zote za umma zilizounganishwa kwenye Mtandao wa Mawasiliano ya Serikali (GOVNET) kwakutumia anuani rasmi ya Baruapepe ya Serikali.

Sifa za Mfumo

Mfumo Huria wa Ofisi Mtandao

 • star
 • star
 • star
 • star
 • star
 • Mfumo huria wa Ofisi Mtandao unatumiwa na taasisi za Umma zilizounganishwa na Mtandao wa Serikali na pia inatumia mfumo wa Baruapepe Serikalini.

  Mfumo huu unahakikisha kuwa data na majalada ya Serikali ni salama na kupatikana kwa watumishi wa Serikali waliopo ofisini.

  Mamlaka inatoa rasilimali za kuhifadhi, kuendesha nakutoa msaada endelevu wa mfumo wa Ofisi Mtandao unaotumiwa na taasisi za Umma kama huduma huria.

  Mfumo huria wa Ofisi Mtandao unatoa GB 200 za uhifadhi.

  Mfumo wa Ndani wa Ofisi Mtandao

 • star
 • star
 • star
 • star
 • star
 • Baadhi ya taasisi zinapenda kuwa na mfumo wa Ndani wa Ofisi Mtandao ili kukidhi mahitaji yao kutokana na kukosa kupata Mtandao wa Serikali.

  Mamlaka inakusanya mahitaji ya mfumo, kutayarisha muundo wa awali na usakinishaji, kukidhi matakwa ya mteja yakiwemo mafunzo.

  Faida za GeOS

 • star
 • star
 • star
 • star
 • star
  1. Inasaidia idadi ya taasisi isiyo na ukomo wala mipaka
  2. Huwapa bila malipo idadi ya watumiaji isiyo na ukomo kwa kila mtumiaji
  3. Mfumo unatoa tafsiri ya wazi na mipaka ya majukumu na fursa
  4. Mfumo wa Ofisi Mtandao unauwezo wa kugawa na kudhibiti majukumu na fursa kwa kila mtumiaji wa mfumo.
  5. Mfumo unaruhusu kukasimu madaraka.

  Tazama Video

  Wasiliana Nasi

  • Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
  • Mamlaka Ya Serikali Mtandao
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao 8 Barabara ya Kivukoni, Jengo la Utumishi
  • S.L.P 4273, Dar es Salaam
  • +255222129868
  • info@ega.go.tz