emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Huduma

Ushauri na Msaada wa Kiufundi

Mamlaka ya Serikali Mtandao inatekeleza lengo la kimkakati la kuratibu, kuwianisha na kuhakikisha utekelezaji wa miongozo na viwango vya Serikali Mtandao kwa taasisi za umma kwa ajili ya kutoa huduma za ushauri na msaada wa kiufundi.

Huduma za ushauri zinafanywa kwa weledi katika fani za Mtandao, Utengenezaji wa mifumo tumizi, usalama, usimamizi wa hazinadata, usimamizi wa mifumo, uchambuzi wa data, uchambuzi wa shughuli za taasisi na usimamizi wa programu.

Aidha, huduma hii inahusisha kuelewa wa mazingira ya utendaji wa taasisi za umma, shughuli za msingi, uendeshaji na dhamira ya pamoja baina ya e-GA na taasisi za umma kwa mfano mapitio ya mfumo.

Kuhusu huduma za ushauri, e-GA inapitia mapendekezo mbalimbali ya Miradi ya TEHAMA, inafanya mapitio ili kupata matokeo, hitimisho na mapendekezo kwa ajili ya kufanya uamuzi kwa kuzingatia viwango na miongozo ya Serikali Mtandao na kanuni nyingine za TEHAMA zinazoelekeza taasisi za umma kwa mfano Mapitio ya mapendekezo ya Miradi ya TEHAMA na Mapitio ya Mahitaji ya Mifumo