emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Huduma

Utayarishaji wa Sera ya TEHAMA

Mamlaka ya Serikali Mtandao inajukumu la kutayarisha mwongozo wa kiwango cha juu kuhusu jinsi TEHAMA itakavyo simamiwa, kuwekezwa, kuendeshwa na kutimiza lengo la kimkakati la taasisi.

Mbinu inayotumika katika kutayarisha Sera ya TEHAMA ni kwamba wataalamu wa TEHAMA wa Mamlaka wananshirikiana na wataalamu wa TEHAMA wa taasisi katika kutayarisha Sera ya TEHAMA. Zana zinazotumika katika kutayarisha Sera ya TEHAMA inahusisha kiolezo(template) cha Mkakati wa TEHAMA (katika Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao), Mipango Mkakati ya muda mrefu na mfupi ya mteja, Kanuni rasmi za uendeshaji (SoPs), Rejesta ya Majanga, Mchanganuo wa Majanga,n.k.

Marejeo ya zana zinazotumika katika utayarishaji wa Sera ya TEHAMA ni Sera ya Taifa ya TEHAMA, Violezo vya Sera ya TEHAMA, Mkakati wa Serikali Mtandao na kanuni nyingine zinazo elekeza TEHAMA Serikalini.