emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Huduma

Utafiti na Mafunzo

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ilianzisha Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (e-GOVRIDC) kwa lengo la kuratibu shughuli za kitafiti, kubuni na kuendeleza jitihada za Serikali Mtandao, ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa umma, kuwajengea uwezo na kukuza vipaji vya vijana wabunifu katika eneo la TEHAMA. Mamlaka inashirikiana Taassisi na Vyuo Vikuu mbalimbali nchini, kwa ajili ya kutambua vipaji na ubunifu kutoka kwa vijana wanaosoma au waliomaliza katika Vyuo Vikuu hivyo.

Kituo hiki kinatoa mazingira wezeshi kwa wanafunzi hao na watafiti mbalimbali katika kufanya tafiti na bunifu mbalimbali zikiwemo za Teknolojia zinazochipukia kama vile Block Chain.