emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Huduma

Usajili wa Anwani za Tovuti za Serikali

Mamlaka ya Serikali Mtandao ni msajili pekee wa majina ya mitandao yote ya .go.tz na .mil.tz. Hivyo, eGA inamamlaka ya kisheria ya kusajili majina yote ya mitandao kwa Taasisi za Serikali. Hii ni katika kutekeleza Sera ya Taifa ya TEHAMA (2003).

Masharti:

  • Fomu ya Usajili wa anwani za tovuti
  • Ada ya Usajili wa anwani za tovuti kwa mwaka ni Tsh. 25,000/=

Taratibu:

  • Jaza fomu ya usajili wa anwani ya tovuti
  • Lipa ada ya usajili wa anwani za tovuti kupitia Akaunti ya Mapato ya Mamlaka (e- Government Authority Revenue A/C) Na.20110002340, NMB Bank.
  • Ambatisha fomu ya usajili wa anwani ya tovuti pamoja na fomu ya kulipia benki
  • Wasilisha fomu hiyo kupitia barua pepe (info@ega.go.tz) au S.L.P 4273 Dodoma.