emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
Tunaimarisha na Kuendeleza Utoaji wa Huduma za Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma

e-GA inakusudia kutekeleza afua mbalimbali ili kusaidia taasisi za umma kutoa huduma mtandao kwa ufanisi. Utekelezaji huo utafanyika kwa kufanya yafuatayo:

 • Uongezaji na uboreshaji wa njia za utoaji wa huduma za serikali mtandao
 • Utoaji wa huduma za ushauri na msaada wa kiufundi
 • Uboreshaji wa uwezo wa rasilimaliwatu katika taasisi,
 • Uwezeshaji wa upatikanaji wa miundombinu na mifumo salama na ya kuaminika ya Serikali mtandao
 • Uimarishaji na uratibu wa jitihada za usalama wa kimtandao katika taasisi za umma.
Tunaimarisha uzingatiaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma

e-GA inalenga kuboresha uratibu na uwianishaji wa utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma kwa kufanya yafuatayo:

 • Uimarishaji wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kwa umma.
 • Utoaji wa Viwango na Miongozo mara kwa mara.
 • Kujenga uwezo wa taasisi za umma kutumia viwango na miongozo katika hatua za kupanga, kuanzisha na kutekeleza jitihada za serikali mtandao.
Tunaimarisha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Jitihada za Serikali Mtandao

e-GA inaimarisha Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (e-GovRIDC). e-GovRIDC ni kitovu cha fikra kinachochukua mkusanyiko na hazina ya teknolojia kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma kwa umma ili kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano inaolenga kuhakikisha TEHAMA inakuwa nyenzo muhimu kufikia uchumi wa habari unaotumiwa na Dunia nzima. Uimarishaji huo utafanyika kwa kufanya yafuatayo:

 • Uimarishaji wa Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao
 • Uimarishaji wa muundo wa ushirikiano katika utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao
 • Kufanya utafiti wa maeneo yenye ushindani wa Serikali Mtandao.