e-GA YATOA VIFAA TIBA KWA WAJAWAZITO

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2025, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imetoa msaada wa vifaa tiba na mahitaji muhimu kwa wajawazito na akina mama waliojifungua, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General) na Hospitali ya Mbagala ya jijini Dar es Salaam. Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja Mawasiliano wa e-GA Bi. Subira Kaswaga alisema, e-GA inatambua umuhimu wa kumuwezesha mwanamke mwenye uhitaji i...