WATUMISHI WAASWA KULINDA AFYA ZAO

Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), wametakiwa kulinda na kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi mara kwa mara, ili kuepukana na hatari ya kupata magonjwa sugu yasiyoambukizwa. Hayo yalisemwa na Dkt. Hafidh Ameir, Afisa anayeratibu Afua za VVU mahali pa kazi ngazi ya taifa, katika sekta ya umma kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Februari 27 mwaka huu, wakati wa kikao cha mwaka cha watumishi jijini Dar Es Salaam....