emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

USHIRIKISHWAJI WA TAASISI ZA UMMA KATIKA KUANDAA NA KUHUISHA VIWANGO NA MIONGOZO YA SERIKALI MTANDAO


USHIRIKISHWAJI WA TAASISI ZA UMMA KATIKA KUANDAA NA KUHUISHA VIWANGO NA MIONGOZO YA SERIKALI MTANDAO


Maafisa TEHAMA kutoka katika taasisi mbalimbali za umma wameshiriki katika kikao kazi cha kuandaa na kuhuisha Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, ili kuhakikisha inaendana na Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019.

Lengo ni kuhakikisha Serikali inakua na Serikali mtandao yenye tija na inayoongeza ufanisa katika utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma.

Kikao hicho kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilifanyika kwa siku 3 kuanzia Agosti 15, 2023 katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijijini Dodoma.

Viwango na Miongozo hiyo inapatikana katika Tovuti ya e-GA kupitia kiungo

https://www.ega.go.tz/standards