Tanzania yashinda Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Ubunifu bora katika huduma za umma kupitia mfumo wa e-Mrejesho.

Tuzo za Umoja wa Mataifa za Ubunifu katika Huduma za Umma 'UN Public Service Innovation Awards' zimetolewa leo Juni 26 mwaka huu, nchini Korea Kusini kwenye Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa 'UN Public Service Week 2024'. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 72 zimeshiriki ambapo mifumo 400 iliwasilishwa na mifumo 15 ukiwemo wa e-Mrejesho ilishinda tuzo mbalimbali ambapo, kutoka Afrika nchi zilizoshiriki na kushinda tuzo hizo...