WATAALAMU WA TEHAMA SERIKALINI WAPEWA MAFUNZO YA AKILI MNEMBA NA UCHAMBUZI WA DATA KUBWA.

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imeratibu na kuendesha mafunzo ya uchambuzi wa Data kubwa ‘Big data analysis’ na Akili Mnemba ‘Artificial intelligence-AI’, kwa wataalam wa TEHAMA kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma, ili kukuza na kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu teknolojia hizo utakaosaidia kukuza ufanisi na kuongeza ubora wa utoaji huduma kwa wananchi.Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo Machi 23 mwaka huu, Meneja Usimamizi...