KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI YAIPONGEZA e-GA KWA UBUNIFU

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kuendeleza tafiti na bunifu zinazochagiza usanifu na utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA inayoleta tija kwa taifa.Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya PAC Mh. Japhet Hasunga, mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara fupi ya kutembelea Kituo Cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGOVRIDC) cha Mamlaka ya Seri...