e-GA YATOA ELIMU KWA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imetoa elimu kuhusu Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa Kamati tendaji ya TEHAMA ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).Lengo la mafunzo hayo ni kuijengea uwezo kamati hiyo juu ya namna inavyoweza kutekeleza ujenzi wa Serikali ya Kidijiti katika taasisi hiyo.Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw.Ramadhani Kailima amesema kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya Maandalizi ya INEC kuelekea ubor...