“GAS MONITORING SYSTEM” MFUMO WA KUFUATILIA KIWANGO CHA GESI KIDIJITALI

MATUMIZI ya nishati safi ya gesi ya kupikia yanazidi kuimarika siku hadi siku. Kuongezeka kwa matumizi haya, kumekiibua Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (e-Government Research, Innovation and Development Centre - eGOVRIDC), kufanya ubunifu kwa kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji wa gesi kidijitali. Mfumo huu ujulikanao kama ‘Gas Monitoring System’, ambao kwa sasa upo katika hatua za majaribio, un...