WATAALAMU WA TEHAMA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZINAZOIBUKIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi Benedict Ndomba amewataka wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kuhakikisha wanasimamia ipasavyo utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kwa kuzingatia matumizi salama, sahihi na yenye kuzingatia matakwa ya kisheria ya teknolojia zinazoibukia. Mha. Ndomba ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kuhusu Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Usimamizi n...



