e-GA YAWEZESHA MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI KUBADILISHANA TAARIFA KIDIJITALI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mha. Benedict Ndomba, amesema kuwa, jumla ya taasisi za umma 109 zimeunganishwa katika Mfumo Mkuu wa Ubadilishanaji taarifa Serikalini ujulikanao kama Government Enterprises Service Bus (GovESB), na tayari mifumo ya TEHAMA 117 imesajiliwa katika mfumo huo.Mfumo wa GovESB, ni mfumo wa kielektroniki unaounganisha mifumo ya TEHAMA ya taasisi za umma iweze kusomana na kubadilishana taarifa kwa usa...