Dkt. Kusiluka Awataka Maafisa TEHAMA Kusimamia Matumizi Salama ya Teknolojia kwa Maslahi ya Taifa

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, amewataka Maafisa TEHAMA nchini kutumia ujuzi wao ipasavyo na kusimamia matumizi sahihi ya teknolojia kwa maslahi mapana ya Taifa. Dkt. Kusiluka ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha sita (6) cha Serikali Mtandao kilichofanyika tarehe 17–19 Februari, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha. Akizungumza katika kikao kazi hicho, Balozi...



