MFUMO WA GMS WARAHISISHA MAWASILIANO SERIKALINI

Mawasiliano kwa njia ya baruapepe ‘email’, yameendelea kushika hatamu duniani ikiwa ni miongoni mwa njia ya haraka ya mawasiliano inayotumika katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za taasisi.Kukua kwa matumizi ya baruapepe, kunatokana na ukuaji wa teknolojia na hivyo, kuwa ni moja ya njia ya haraka na inayoaminika katika mawasiliano rasmi ya kiofisi.Ili kuhakikisha Serikali inapiga hatua katika matumizi ya baruapepe, Mamlaka ya Serikali Mtanda...