π²-ππ π¬πSHIRIKIANA NA π¦πππ§π π¬π πππππ π’ πUIMARISHA π πππ¨π π’ π¬π πππππππ§πππ

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imeendelea kushirikiana na Wizara ya Kilimo katika kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali inayorahisisha utoaji wa huduma, kuongeza uwazi na kuboresha usimamizi wa shughuli mbalimbali za kilimo nchini. Akizungumza katika Maonesho ya kitaifa ya wakulima ‘Nanenane’ yanayoendelea jijini Dodoma, Meneja Mawasiliano wa e-GA, Subira Kaswaga, amesema e-GA imekuwa ikibuni na kusimamia mifumo ya TEHAM...



