Baraza la wafanyakazi e-GA lajengewa uwezo

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba, amewataka wajumbe wa Baraza kuendesha vikao vya Baraza kwa tija na ufanisi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya usimamizi na uendeshaji wa vikao hivyo. Ndomba amesema hayo Novemba 21 mwaka huu jijini Dodoma, wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza la tano (5) la Wafanyakazi wa Mamlaka, kilichofanyika sambamba na mafunzo ya uendeshaji wa baraza hilo. A...







