Kamati Baraza la Wawakilishi yaipongeza e-GA kutumia wataalamu wa ndani Ujenzi na Usanifu Mifumo ya TEHAMA Serikalini.

Kamati Baraza la Wawakilishi ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC), imeiopongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kwa kutumia wataalamu wa ndani katika ujenzi na usanifu wa mifumo ya TEHAMA Serikalini. Pongezi hizo zimetolewa hii leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh.Juma Ali Khatib, baada ya kupokea wasilisho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mhandisi Benedict Ndomba, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya e-GA...







