VODACOM TANZANIA YATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI NA UBUNIFU CHA e-GA.

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGOVRIDC) cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), jijini Dodoma na kufanya mazungumzo na e-GA kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.Ziara hiyo ya Vodacom ililenga mambo muhimu matatu, ikiwemo kufahamu shughuli na jitihada mbalimbali za e-GA kwenye eneo la utafiti...