e-GA IMELETA MAGEUZI YA KIDIJITALI SERIKALINI: DKT. SAID MOHAMMED KATIBU MTENDAJI NECTA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohammed, ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa jitihada inazofanya, katika mageuzi ya kidijitali Serikalini, jambo ambalo limechangia kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Dkt. Mohammed amesema hayo hivi karibuni ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya mahojiano maalum na mwandishi wetu kuhusu mchango wa e-GA katika mapinduzi ya kidijitali kwenye ta...