emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Zingatieni Sheria na Miongozo ya Serikali Mtandao- Turuka


Zingatieni Sheria na Miongozo ya Serikali Mtandao- Turuka


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka amewataka Watendaji Wakuu wa Taasisi za umma pamoja na viongozi wengine walio katika ngazi ya uamuzi kutekeleza malengo mbalimbali ya Serikali Mtandao kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo na inayoendelea kutolewa  ili kutoa huduma kwa umma kwa uwazi, haraka na kwa ufanisi.

Dkt. Turuka aliyasema hayo alipokuwa anafunga Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Serikali Mtandao kwa washiriki wa kundi la pili uliofanyika jijini Arusha Agosti 19 na 20, 2015.

 “Katika muda wa siku mbili za uwepo wenu hapa, mmeona changamoto mbalimbali za utekelezaji wa Serikali Mtandao, hivyoni wajibu wa kila mtendaji kuziweka katika mipango ya taasisi yake ili zitatuliwe na hatimaye kutoa huduma bora kwa umma” alisema Turuka.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi Agosti 19, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na kumalizika Agosti 20, 2015 jijini Arusha. Malengo ya Mkutano huo ni Kujenga uwezo na ushirikiano katika kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania, Kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizoko katika utekelezaji wa Serikali Mtandao  utakaosaidia kuleta  maendeleo zaidi ya kiuchumi na kijamii kwa kuimarisha utoaji huduma kwa umma kwa kutumia TEHAMA na Kuongeza ufahamu na kushirikiana maarifa na kukuza uhusiano wa kikazi na wataalam wengine wa Serikali Mtandao kutoka nchi zinazofanya vizuri katika utendaji wa Serikali Mtandao