NAIBU WAZIRI AITAKA e-GA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Clement Sangu (Mb), ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi, ili kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wabunifu kwenye eneo la TEHAMA. Mhe. Sangu ametoa rai hiyo hivi karibuni, wakati akifunga programu ya awamu ya tano ya mafunzo kwa vitendo (practical training) pamoja na mafunzo kazini (internship) kwa mwaka wa fedha 2...