TUKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI: e-GA

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imeahidi kushirikiana na Benki ya NMB ili kuimarisha, kukuza na kuendeleza ujuzi na vipaji kwa vijana wa Kitanzania wabunifu na wale wanaosoma fani ya TEHAMA, katika Vyuo Vikuu mbalimbali nchini, kupitia programu maalum ya mafunzo kwa vitendo inayotolewa na e-GA kupitia Kituo chake cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGOVRIDC).Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa e-GA M...