MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO (e-GA) NA CHUO KIKUU MZUMBE WASAINI HATI YA MAKUBALIANO (MOU) KUIMARISHA SEKTA YA TEHAMA NCHINI

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Chuo Kikuu Mzumbe, wamesaini hati ya makubaliano (MOU) ya ushirikiano katika masuala ya elimu, utafiti, na maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ikiwa ni hatua inayolenga kuimarisha na kukuza tasnia ya TEHAMA ili kuboresha jitihada za Serikali Mtandao sambamba na kuimarisha uhusiano uliopo katika taasisi hizo.Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, imefanyika hivi karibuni katika ofis...