OFISI YA TAIFA YA MASHITAKA YATAKIWA KUTUMIA MIFUMO YA TEHAMA KUIMARISHA UTOAJI HAKI KWA WANANCHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, amewataka watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS) kutumia Mfumo wa Kielktroni wa Usimamizi na Uendeshaji wa Kesi za Jinai ujulikanao kama ‘Case Management Information System’ (CMIS), ili kuimarisha utendaji kazi na utoaji haki kwa wananchi. Simbachawene alitoa kauli hiyo jana wakati akikabidhi mfumo wa CMIS na tovuti ya O...







