Badilisheni Mtindo Wa Maisha Kulinda Afya Zenu

Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wametakiwa kubadili mtindo wa maisha ili kuwa na afya bora. Hayo yamesemwa na Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Eric Kalembo katika zoezi la upimaji afya za watumishi lililofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao, jijini Dar Es Salaam. Bw. Kalembo amesema kuwa Idadi kubwa ya watumishi wa Mamlaka ni vijana ambao ni chachu ya maendeleo ya Taifa hivyo wanapaswa kuwa na afya bor...