WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA KULETA MAGEUZI YA KIDIJITALI SERIKALINI

Wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo katika tasnia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), wametakiwa kuwa wabunifu katika kutumia teknolojia mpya zilizoibuka duniani ili kuongeza ufanisi na kuleta tija katika utendaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mha. Benedict Ndomba, wakati akifungua mafunzo ya awamu ya tano katika Kituo cha Ut...