Mtumishi Mahiri e-GA 2023: MWANAASHA SEMBOKO

Afisa TEHMA Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Huduma za TEHAMA Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bi. Mwanaasha Semboko ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kumchagua Mtumishi Mahiri wa Mamlaka kwa mwaka 2023.Hayo yalibainishwa na Meneja wa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Bw. Erick Kalembo wakati wa mahojiano na mwandishi wetu jijini Dar Es Salaam kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2...