TAASISI NA HALMASHAURI ZAENDELEA KUNEEMEKA NA MFUMO WA e-BOARD

Taasisi na Halmashauri mbalimbali nchini zimeendelea kuunganishwa na kunufaika na matunda ya ubunifu ya wataalamu wa ndani yatokanayo na mfumo wa e-Board.Uanzishwaji wa mfumo huu ni Juhudi za Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) za kuhakikisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yanaimarishwa ili kuboresha utendaji kazi wa Taasisi za Umma nchini.Mfumo wa eBoard ni mfumo unaoratibu vikao vya Bodi, Kamati za Bodi...







