WAZIRI BASHE AZINDUA MFUMO WA MUVU

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe, amezindua Mfumo wa kielektroniki wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) unaowezesha na kurahisisha uhamasishaji, usimamizi na uendeshaji wa Vyama vya Ushirika kidijitali. Uzinduzi huo ulifanyika hivi karibuni wakati wa kilele cha maadhisho ya siku ya ushirika duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane Ipuli Mjini Tabora, na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi pamoja na waandish...







