Ndejembi aitaka e-GA kuendeleza utafiti na ubunifu wa Mifumo ya TEHAMA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kuendelea kufanya utafiti na ubunifu wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuibua Mifumo itakayosaidia kuimarisha sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji ili kuleta maendeleo kwa taifa.Mhe. Ndejembi ametoa wito huo wakati akifungua kikao kazi cha tatu cha Serikali Mtandao ki...







