e-GA YAKABIDHI KOMPYUTA 10 KWA JESHI LA POLISI

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imetoa mchango wa kompyuta 10 kwa Jeshi la Polisi nchini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika utoaji wa haki kwa wananchi.Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika Ofisi za Mamlaka jijini Dar es Salaam ambapo kwa upande wa e-GA Bw. Benjamin Dotto Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwezeshaji wa TEHAMA alikabidhi komputa hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Mhandisi. Benedict Ndomba.Akiongea wakat...







