UJENZI WA MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI

Meneja wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ACP. Raphael Rutaihwa amehimiza Vitengo vya TEHAMA Serikalini kufuata Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao ili kujenga mifumo bora na yenye tija.ACP. Rutaihwa amesema hayo wakati akitoa elimu kwa umma kuhusu Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 na kanuni zake.“Ni vyema kila taasisi ya umma kuhakikisha inafuata Sheria, Kanuni, Viwango na Mio...







