Utafiti na Ubunifu Suluhisho kwa Serikali Mtandao

Wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo wameaswa kufanya utafiti na kuwa wabunifu katika masuala ya Serikali Mtandao ili kupata mifumo ambayo ni suluhisho la changamoto zilizopo katika jamii.Kauli hiyo imetolewa Septemba 12, 2022 jijini Dodoma wakati Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akifunga programu ya nne ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu k...







