USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA SERIKALI MTANDAO UNAVYOCHOCHEA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA TEHAMA SERIKALINI

Ufanisi wa Serikali Mtandao hutegemea usimamizi mzuri wa rasilimali, ushirikiano wa wadau, na utekelezaji wa mikakati madhubuti ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora, kupunguza urasimu, na kuongeza uwazi, na hatimaye kuboresha maisha ya wananchi.Katika kuhakikisha usimamizi thabiti wa Serikali Mtandao nchini, Kifungu cha 15 cha Sheria ya Serikali Mtandao Namba 10 Sura ya 273 ya Mwaka 2019 (Sheria), kinaelekeza juu ya uanzishwaji wa muundo na...