MIAKA 10 YA MFUMO WA BARUAPEPE SERIKALINI (GMS), WADAU WAFURAHISHWA NA UHAKIKA WA MAWASILIANO SALAMA SERIKALINI

Lilianza kama wazo, kisha wataalamu wakaketi na kutengeneza mfumo wa Baruapepe za Serikali (Government Mailing System - GMS), ambapo sasa umetimia muongo mmoja wa mafanikio ya matumizi ya mfumo huu. Kwanini tusijenge mfumo wa baruapepe za Serikali, ili kila mtumishi wa umma aweze kufanya mawasiliano ya kiofisi kupitia mfumo huu? Hili ndilo swali lililoifanya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kusanifu na kujenga mfumo wa GMS mwaka 2014. Dh...