USHIRIKIANO WA TPA NA e-GA WACHOCHEA MATUMIZI YA TEHAMA BANDARINI

Ushirikiano uliopo kati ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), umechangia kukua kwa matumizi ya Serikali Mtandao katika uendeshaji wa shughuli za bandari na utoaji wa huduma kwa wananchi. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa TEHAMA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Abdulatif Minhajj, hivi karibuni wakati alipofanya mahojiano maalum na mwandishi wetu kuhusu mchango wa e-GA katika...