WAKUU WA TAASISI ZA UMMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

Wakuu wa Taasisi za Umma wametakiwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi ya utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao, ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa TEHAMA katika taasisi zao ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia yanayoibuka mara kwa mara.Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Ridhiwani Kikwete (Mb), wakati akifunga Kikao Kazi cha Nne cha Serikali Mta...