TENGENI MUDA WA MAISHA BINAFSI KUEPUKA UGONJWA WA AFYA YA AKILI: DR. KWEKA

Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA). wametakiwa kutenga muda wa kutosha kwa ajili ya masuala mbalimbali yanayohusu maisha binafsi, ili kujiepusha na msongo wa mawazo unaoweza kusababisha matatizo ya afya ya akili.Wito huo umetolewa hivi karibuni na Daktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Garvin Kweka, wakati akitoa elimu ya afya ya akili kwa watumishi wa Mamlaka katika kikao cha watumishi kilichofanyika jijini Dar es S...