Afya Bora Huongeza Ufanisi Kazini: Dkt. Hafidh

Na. Catherine Peter Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), wametakiwa kulinda afya zao ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kazini. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Dkt. Hafidh Ameir, Afisa anayeratibu Afua za VVU mahali pa kazi ngazi ya taifa, katika Sekta ya Umma kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), wakati wa kikao cha mwaka cha watumishi wa e-GA kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Maji...



