MIAKA 3 YA RAIS DKT. SAMIA: SERIKALI MTANDAO YAZIDI KUIMARIKA

Ilianza siku na hatimaye miaka mitatu sasa imetimia tangu Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuingia madarakani.Ilikua Ijumaa ya Machi 19 mwaka 2021, siku ambayo historia iliwekwa kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuapishwa rasmi na Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania, kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuanza kuongoza rasmi Serikali ya Aw...