Waziri Kikwete Asisitiza Matumizi ya e-Mrejesho, Aipongeza e-GA.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amewataka wananchi kuendelea kutumia mfumo wa e-Mrejesho katika kutoa pongezi, malalamiko na maoni kwa taasisi za umma na kisha kupata mrejesho wa utekelezaji. Akizungumza hivi karibuni na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mhe.Ridhiwani alisema kwamba, utoaji wa maoni ya mara kwa mara ni jambo muhimu katika kuboresha utoaji huduma kw...







