emblem
Mamlaka ya Serikali Mtandao
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Warsha ya siku mbili ya kujadili matumizi na umuhimu wa teknolojia ya ‘Blockchain’ pamoja na Sarafu Mtandao (Techcon Tanzania 2024) imeanza leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.Warsha hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kwa kushirikiana na Chama cha Umoja wa Blockchain Afrika (UABA) ambapo taasisi mbalimbali za umma na binafsi zikiwemo benki, zinashiriki katika warsha hiyo.

Soma Zaidi

Taasisi za umma nchini, zimetakiwa kuwahimiza wadau wake kutumia mfumo wa e-Mrejesho kuwasilisha kero na maoni mbalimbali sambamba na taasisi hizo kuhakikisha zinashughulikia maoni na kero hizo kwa wakati, kupitia mfumo wa e-Mrejesho ili kuendelea kujenga imani kwa wadau wake.Wito huo umetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bi. Subira Kaswaga, wakati wa Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama ‘Sabasaba’...

Soma Zaidi

Tanzania imeshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Ubunifu katika Huduma za Umma kwa mwaka 2024 ‘UN Public Service Innovation Awards’ kupitia mfumo wa e-Mrejesho, ambao umetambuliwa na umoja huo kama jukwaa linalowezesha serikali kukusanya maoni na malalamiko ya wananchi kwa njia ya kidijitali, na hivyo kufanya maamuzi ya sera na utekelezaji kwa wakati.Hafla ya utoaji wa tuzo za Umoja wa Mataifa kuhusu Huduma za Umma imefanyika Juni 26 mwaka huu waka...

Soma Zaidi

Watu wengi hupoteza mafaili yao muhimu mara tu simu au kompyuta zao zinapoharibika au kupotea, huenda hata wewe ukawa ni miongoni mwa waathirika hao. Habari njema ni kuwa mwarobaini wa tatizo hili umepatikana, na sasa mafaili yako yatakuwa salama hata kama utapoteza simu au kompyuta yako kuharibika.Naam! Ni kupitia mfumo wa kuhifadhi mafaili yako mkondoni wa ‘Twiga Cloud’ unaweza kutunza mafaili yako wakati wowote na kuwa na uhakika wa usalama wa...

Soma Zaidi

“Uadilifu na ubunifu kwa utoaji wa huduma bora kwa umma” huu ndio moto wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), unaoangaza njia inayochochea bunifu mbalimbali za TEHAMA zitakazosaidia kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kidijitali.Ili kufikia mafanikio haya, Oktoba 2019 e-GA ilianzisha Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGOVRIDC), kwa lengo la kuimarisha na kukuza tafiti pamoja na bunifu za TEHAMA, kwa kushirikiana na...

Soma Zaidi
Mpangilio